Karibu katika tovuti ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tegeta. Tovuti hii inakusudia kukupatia wewe mtembeleaji wetu taarifa za hakika na maarifa ya kuaminika yatakayokusaidia kuchukua hatua za mabadiliko katika maisha. Tumekuandalia mambo mengi ambayo hayatakuchosha, mambo yatakayokusaidia kuanzisha na kukuza mahusiano na Yesu aliye "Alfa na Omega, mwanzo na mwisho . . . aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. (Ufunuo 1:8).
Yesu anakupenda, naye anatamani kufanya urafiki na wewe. Yeye amekuandalia makao ya milele mbinguni. Hivi karibuni atakuja kukuchukua ili ukaishi naye milele zote. Chagua kumpa nafasi katika maisha yako leo. Mungu akubariki.
KARIBU SANA NA MUNGU AKUBARIKI