UTANGULIZI
Mtaala huu ni mali ya Tanzania Union Mission - toleo la Mtaala wa Biblia. Ni kozi ya Biblia kwa muda wa miaka 13 ambayo imeandaliwa kukidhi mahitaji ya mafundsidho ya dini kuanzia shule za awali hadi elimu za sekondari (kidato cha nne).
Kozi hii imeganywa katika ngazi tatu:
1. Miaka miwili ya Elimu ya Awali
2. Miaka saba ya Elimu ya Msingi
3. Miaka minne ya Elimu ya Sekondari
Kozi hii itakuwa inatolewa kwa kuendelea (spriral system) kwa sababu mada zinategemeana na zimerudiwa katika ngazi mbalimbali kwa kuingia ndani zaidi. Mtaala huu umekusudiwa pia kutumika kfundishia vijana wa kiadventista wanaosoma katika shule zisizo za kanisa. Kwa kuwa fildi na konferensi zinaweza zisifanikiwe kuwa na walimu wa kutosha kufundisha wanafunzi katika shule zisizo za kanisa, inashauriwa kuunganisha darasa la kwanza na la pili, la tatu na la nne, la tano, la sita na la saba, kidato cha kwanza na cha pili na kidato cha tatu na cha nne. Sehemu ya kidato cha tatu na cha nne ya mtaala huu ina mada ambazo zimelenga kuwaanda wanafunzi kwa ajili ya kufanya mtihani wa kidato cha nne wa Biblia uitwao Bible Knowledge (Maarifa ya Biblia).
TATHMINI YA MAHITAJI
1. Maandiko Matakatifu ni kipimo kikamilifu cha ukweli na kwa hiyo yanapaswa kupewa nafasi ya juu sana katika elimu. “Ili kupata elimu inayostahili jina (la Mungu), ni lazima tumjue Muumbaji na Kristo Mkombozi kama wanavyofunuliwa katika maneno matakatifu” (Education, uk.27).
2. Elimu haikamiliki bila dini kama kitu cha kuidhibiti. Ni lazima ijengwe juu ya Maandiko Matakatifu.
3. Mitaala katika shule zetu ni lazima imfanye Mungu kuwa kiini cha elimu hiyo na Biblia kikiwa kitabu kinachoongoza mambo yote ya elimu.
4. Mtaala huu umeingiza maadili ya kiafrika yanayofaa kwa kutumia mifano ya kufundishia kutoka katika jamii mbalimbali za kiafrika.
UMUHIMU WA MTAALA HUU
Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataishahu hata atakapokuwa mzee, (Mithali 22:6).Kwa hiyo, ni wajibu wa kila mhusika anayejali, awe mzazi, shule, makanisa na walimu kufanya kazi kwa pamoja ili kutoa mafundisho yanayofaa kwa vijana. Mafundsiho yatakayowawezeaha kuwa watenda kazi wenza pamoja na Kristo na yatakayowandaa kwa ujio wake (Yesu) wa mara ya pili. “Kwa jeshi hilo la watenda kazi kama vijana wetu, wakiwa wamefundishwa kwa usahihi, watatoa kwa haraka kiasi gani ujumbe wa Mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka na anyekuja upesi, ujumbe unaweza kupelekwa katika dunia yote”. (Ellen White, 1943, uk. 555).
Mtaala huu utakuwa mwongozo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mada zinazofundshwa zinafanana na zinakubaliana na mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wasabato.
NAMNA YA KUTUMIA MTAALA HUU
Wakurugenzi wa Elimu wa Konferensi na Fildi watahitajika:
- Kuwa waratibu wakuu wa mtaala
- Kuwasimamia na kwasaidia walimu wa Biblia walei
- Kuteua wakufunzi/walimu wa kusaidia kazi ya kufundisha
- Kuendesha mafunzo kwa walimu walei
- Kujadili na walimu juu ya mada ngumu
- Kupata mrejesho kutoka kwa wote wanaotumia mtaala huu
- Kusaidia katika kufanya marekebisho ya mtaala kwa kuzingatia mapendekezo, mafanikio na matatizo yatokanayo na matumizi ya mtaala
Mtaala huu utatumika kwa majaribio kwa muda fulani na kwa hiyo maoni ya kuuboresha yanakaribishwa ili kuufanya uwe rahisi zaidi kuutumia.
MALENGO YA MTAALA
Malengo yaliyoorodheshwa hapa chini ni ya jumla na yanahusu mtaala mzima. Walimu wanategemewa kuwa na malengo mahsusi kwa kila mada inayofundishwa. Lengo la kwanza kabisa kwa mwalimu linapaswa kuishi maisha ambayo yatakuwa kielelezo cha misingi ya biblia anayayoifundisha kwa wanafunzi. Kila mada inapomalizika inapaswa kutoa fundisho la kiroho kwa wanafunzi.
Inatarajiwa kuwa mwisho wa kozi hii ya kina, wanafunzi wataweza:
- Kumuelewa Mungu kama nafsi ambaye wanaweza kumjua
- Kuielewa Biblia kama njia ya kumjua Mungu
- Kufahamu ufunuo wa ukweli juu ya Mungu kupitia kila tukio lililoandikwa na kila fundisho
- Kuyaelewa maandishi ya Ellen G.White kama ushuhuda mwingine juu ya ukweli kuhusu Mungu
- Kufahamu kuwa kusudi la ibada ni ili tuwe zaidi na zaidi kama Kristo tunayempenda
- Kuwa na uelewa wa misingi 28 ya imani ya Kanisa la Waadventista Wasabato
- Kufahamu asili ya uasi ambao umetokea ulimwenguni, mabadiliko ambayo uasi huu umeleta ulimwenguni pamoja na suluhisho na uasi huo ambalo linapatikana kwa kumjua Mungu.
- Kujifunza kwamba kushiriki imani yao na watu wengine itakuwa ni namna ya asili ya kukuza uelewa wao juu ya Mungu
- Kutambua kuwa Mungu aliyeumba ulimwengu ulio huru amewapatia upendeleo na wajibu wa kufanya uchaguzi wao wenyewe. Kwa hiyo wanaonyesha kama wanaweza kuaminiwa kwa kuwa na uhuru na uzima wa milele
- Kuwa na uelewa wa ujumbe wa afya kama sehemu ya muhimu ya Mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wasabato
- Kuelewa asili ya Mwanadamu: Mwanadamu aliyeanguka na anayehitaji kurejeshwa katika sura ya Mungu, Yohana 3:16
NJIA ZA KUFUNDISHIA NA SHUGHULI ZA KUFANYA
Njia za kufundisha zitakuwa tofauti wakati wote, kutegemeana na mwalimu, mada, aina ya wanafunzi na darasa walilofikia. Hata hivyo, hapa chini kuna mifano michache ya njia ambazo zinatumiwa mara nyingi na walimu na kwa kiasi Fulani zimebainika kuleta ufanisi.
1.a Ufundishaji wa moja kwa moja
Hii ni kanuni ya ufundishaji ambapo mwalimu ndiye mtoaji mkuu wa maarifa. Mwalimu huhamisha kweli fulani kutoka kwake kwenda kwa wanafunzi kwa nia ya moja kwa moja kwa kadri inavyowezekana. Tofauti na njia ya kutoa mhadhara, katika njia hii ya ufundishaji wa moja kwa moja mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa wakati wa kufundisha kutakuwa na mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi yanayohusisha maswali na majibu, marudio na mazoezi na masahihisho.
Faida kubwa za njia ya ufundishaji wa moja kwa moja ni kwamba:
(i) Ni njia iliyo na mwelekeo wa kitaaluma zaidi ambapo mwalimu huelekeza, kutawala na kupunguza muda wa mwanafunzi kujifunza.
(ii) Hutoa nafasi kwa mwalimu kufuatilialia uelewa wa mwanafunzi kwa sababu mwalimu huwasilisha mada yake kwakwa hatua zilizopangiliwa na kwa kawaida ataenda kwenye hatua inayofuata baada ya wanafunzi kuielewa hatua iliyopita
1.b Mchezo-kielelezo
Hii ni njia ya ufundishaji ambapo wanafunzi darasani wanachaguliwa ili kuigiza halifulani huku wanafunzi wenzao wakiwaangalia na kuchukua masuala fulani ya mchezo kwa kufuata maelekezo ya mwalimu. Njia hii ni nzuri lakini haitumiki sana na inahitaji muda wa kutosha na maandaalizi yaliyopangaliwa vizuri. Mchezo kielelezo, usipopangailiwa vizuri, unaweza kuishia kuwa maburudisho badala ya kuwa njia ya kufundishia. Kwa maneno mengine, wanafunzi wanaweza wasipate maarifa yaliyokusudiwa na mwalimu anaweza asifikie malengo yaliyokusudiwa.
Mchezo-kielelezo huwaweka wanafunzi katika mazingira halisi ya tukio au shughuli husika. Kwa mfano, wanaweza kuigiza kisa cha Yusufu na ndoto zake, wanawali kumi, mwana mpotevu n.k. Kwa hiyo, pale inapowezekana, mwalimu atumie njia hii. Ili kufanikiwa kufikia malengo ya somo yaliyokusudiwa, mchezo kielelezo ni lazima upangiliwe na kuandaliwa vizuri.
1.c Kusimulia visa
Ufundishaji kwa njia ya kusimulia visa ni njia yenye yenye mafanikio makubwa hasa ikitumika kwa wanafunzi wa elimu ya Awali na Msingi. Hata hivyo, mwalimu ni lazima ajipange na kuandaa vizuri mada yake ili kisa kiwe hai na kivutie. Matumizi ya lugha rahisi na vielelezo kutoka katika mazingira yao na shghuli za kila siku ni muhimu sana. Kwa visa rahisi vya biblia, mwalimu awape kazi ya kuvisoma wao wenyewe kutoka kwenye Biblia na kisha kuvisimulia kwa wanafunzi wenzao darsani.
1.d “Project”
“Project”zinaweza kufanywa na mwanafunzi mmoja au kikundi. Mwalimu anapaswa kutoa maelekezo yanayoeleweka vizuri juu ya nini wanafunzi wanatakiwa kufanya. Baadhi ya project zinaeza kuwa:
i. Vikundi vya maombi
ii. Mikutano maalum ya kidini (retreats)
iii. Kutembelea kanisa jingine au shule nyingine
iv. Ushuhudiaji
v. Kwaya
Shughuli hizi zote zinaweza kusaidia kukuza hali ya kiroho ya wanafunzi. Kwa ajili ya ufanisi, shughuli hizi ni lazima ziratibiwe vizuri na mwalimu.
1.e Mijadala
Itapendeza kama kutafanyika mjadala baada ya wanafunzi kusoma mada fulani iliyoandaliwa. Mjadala unaweza kufanyika katika vikundi vya watu wachache na baadaye kila kikundi kikawasilisha yale yaliyojadiliwa. Katika maandalizi ya mjadala, ni muhimu mwalimu aandae maswali mahususi kwa ajili ya majadala husika na ausimamie vizuri mjadala huo. Kwa:
i. Kupanga dakika zitakazotumika kwa ajili ya mjadala
ii. Baada ya mjadala, kila kikundi kipewe muda wa kuwasilisha waliyojadili
iii. Mwalimu ahitimishe mjadala kwa kutoa muhtasari wa yaliyojadiliwa na kutoa majibu ya maswali yaliyokuwa yanajadiliwa
1.f Kupaka rangi
Upakaji rangi ni njia nyingine ya kujifunza inayowavutia wanafunzi hasa wa shule za awali na msingi. Pale inapowezekana, wanafunzi wapewe kazi ya kupaka rangi picha zinazowakilisha kisa fulani cha Biblia.
Sambamba ba njia hizi za ufundishaji, ushauri ufuatao unaweza kumsaidia mwalimu:
- Kila somo la Biblia lianze kwa ombi na kuhitimishwa kwa ombi
- Kila somo lazima lihitimishwe na kitu cha kujifunza kiroho
- Biblia itumike kwa kila somo la Biblia na wanafunzi wapewe fursa ya kufanya rejea na kusoma katika Biblia zao wenyewe
- Mwalimu ajitahidi kutumia vifaa vinavyosaidia kufundisha kama vile overhead Over head projector, ramani, picha n.k
- Mwalimu aepuke kuhubiri bali afundishe
Kwa jaili yoyote ya ufundishaji itakayotumika, walimu waadventista ni lazima waige mfano wa Mwalimu mkuu (Yesu) kama kielelezo cha ufundishaji. Aliishi maisha yanayoendana na kile alichofundisha. Misingi mikuu katika ufundishaji wake ilizingatia: upendo, wema, uvumilivu, unyenyekevu na haki.
ELIMU YA AWALI
MWAKA WA KWANZA
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
REJEA Sura na kurasa zilizoonyeshwa ni katika vitabu vya kiingereza |
WIKI YA 1 |
Mungu:
|
|
WIKI YA 2 |
Baraka za Mungu
|
|
WIKI YA 3-6 |
Hapo Mwanzo
i. Siku ya kwanza na pili ii. Siku ya tatu nay a nne iii. Siku ya tano nay a sita iv. Siku ya Saba
|
Mwanzo 1:5 Wazee na Manabii sura ya 2, 47 na 48 Mathayo |
WIKI YA 7 |
Bustani ya Edeni: a. Bustani iliyo nzuri b. Adamu na Hawa wakifanya kazi bustanini c. Mahali pa kukutania na Mungu d. Amri na maelekezo ya Mungu |
Mwanzo 2 |
WIKI YA 8 |
a. Lusifa, malaika mkuu na mzuri b. Nafasi ya Lusifa mbinguni c. Anguko la Lusifa
|
Wazee na Manabii sura ya 36-43 Story of Redemption sura ya 13-18 Tumaini Kuu 496-498,500. |
WIKI YA 9 - 10 |
Muongo mkuu: a. Adamu na Hawa wadanganywa b. Adamu na Hawa wavunja amri ya Mungu c. Wafukuzwa bustanini d. Mungu awafanyia nguo |
Ufunuo 12:7- 9 Wazee na Manabii uk. 41-43 Story of Redemption uk. 17-19 Tumaini Kuu uk. 498-500 |
WIKI YA 11 |
a. Watoto wa kwanza kuzaliwa duniani: Kaini na Habili b. Kazi za Kaini na Habili c. Kaini amuua ndugu yake Habili – mtu wa kwanza kufa d. Matokeo ya dhambi |
|
WIKI YA 12 |
Henoko: Mtu aliyetembea na Mungu: a. Henoko alikuwa nani? b. Henoko alienda pamoja na Mungu c. Henoko alitwaliwa na Mungu d. Tunaweza kuenda pamoja na Mungu |
Mwanzo 5 Wazee na Wafalme sura ya 6 Story of Redemption sura ya 7 |
WIKI YA 13 |
Safina ya kwanza kujengwa duniani: a. Nuhu aambiwa na Mungu kujenga safina b. Nuhu ahubiri kwa miaka 120 c. Mungu aleta mvua kubwa na mafuriko d. Nuhu na familia yake waokolewa pamoja na wanyama waliochaguliwa c. Upinde wa mvua |
Wazee na Manabii uk. 95 - 97 Story of Redemption uk. 64 Mwanzo sura ya 6 hadi 9 |
WIKI YA 15 |
a. Jengo la kwanza la ghorofa duniani b. Mungu awatawanya wajenzi wa ghorofa |
Mwanzo sura ya 11 |
WIKI YA 16-18 |
a. Isaka: Mtoto wa pekee wa Abrahamu b. Esau na Yakobo: Watoto wa Isaka c. Esau auza uzaliwa wake wa kwanza d. Yakobo amdanganya baba yake ili kupata mibaraka e. Ndoto ya Yakobo: Ngazi ndefu f. Yakobo apigana na malaika |
|
WIKI YA 19-20 |
Familia ya Yakobo: a. Watoto 12 wa Yakobo b. Yusufu:Mtoto anayependwa c. Ndoto za Yusufu d. Yusufu auzwa na nduguze |
Mwanzo 37:1-36 Wazee na Manabii uk. 209 -231
|
ELIMU YA AWALI
MWAKA WA KWANZA
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-2 |
Kisa cha Yesu: a. Yusufu na Mariamu: wazazi waYesu b. Yesu azaliwa katika hori la ng’ombe c. Malaika watoa taarifa d. Mamajusi wa Mashariki |
Mathayo sura ya 1 |
WIKI YA 3 |
a.Mtoto Yesu akimbizwa Misri kwa usalama b.Safari ya kurudi Nazareti |
Mathayo sura ya 2 |
WIKI YA 4 |
a.Yesu aenda hekaluni na wazazi wake b.Yesu abaki hekaluni na kutoonekana kwa siku 3 |
Luka sura ya 2:41-52 |
WIKI YA 5 |
a.Yesu abatizwa b. Yesu ajaribiwa na shetani |
Mathayo sura ya 3 na 4 |
WIKI YA 6-7 |
a. Yesu: Rafiki wa watoto b. Yesu:Tabibu mkuu c. Yesu ashtakiwa na kusulubishwa |
Mathayo sura ya 4 |
WIKI YA 8-10 |
Kuzaliwa kwa Samweli:Kijana mdogo aliyeitwa kumfanyia Mungu kazi a. Ombi la mama ili kupata motto b. Kuzaliwa kwa Samweli c. Hanna amtoa Samweli kwa Mungu d. Samweli aitwa na kuongea na Mungu |
Samweli sura ya 1-3 Wazee na Manabii uk. 569-573 |
WIKI YA 11-14 |
Daudi:Mvulana mchungaji a. Maisha ya Daudi kama mchungaji b. Daudi na Goliathi c. Daudi na Yonathani |
Wazee na Manabii uk. 635-648 1 Samweli sura ya 16-20 |
WIKI YA 15-18 |
a. Mtu mkubwa mfupi b. Mara 490 na zaidi c. Nyumba juu ya mwamba d. Nuru na chumvi e. Taa ndogo kumi |
Luka sura ya 19 Mathayo sura ya 25 |
WIKI YA 19-20 |
Mfalme kijana mwenye hekima:Sulemani Kuishi maisha yenye afya |
1 Wafalme 3:17 – 22 Wazee na Manabii uk. 750-755 Wazee na Wafalme uk.25-50 1 Mambo ya Nyakati sura ya 28 na 29 2 Mambo ya Nyakati sura ya 1,6, 7:1-4 |
SHULE YA AWALI
MWAKA WA PILI
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-2 |
a. Kuzaliwa kwa Musa b. Musa afichwa pembeni mwa mto c. Musa aokotwa na binti Farao d. Musa katika nyumba ya Farao e. Musa akimbia kwa Farao |
Kutoka Wazee na Manabii uk. 241-244 Matendo 7:22-29 Wazee na Manabii uk. 247 -265 |
WIKI YA 4-5 |
a. Musa mchunga kondoo b. Kichaka kinachoungua c. Musa arudi tena Misri |
Kutoka 4:27-31; 5,6 Wazee na Manabii uk.257 - 265 |
WIKI YA 6-9 |
Waache watu wangu waende: a. Vyura,chawa, mainzi, magongwa, majipu, mvua yam awe, nzige na giza c. Kutoka Misri d. Kuvuka bahari ya Shamu |
Kutoka 8, 9:1-7, 9:8-35 Wazee na Manabii uk.265 -287 Kutoka sura ya 11, 12, 13, 14 Wazee na Manabii uk.287 -296 Zaburi 104:33 |
WIKI YA 10 |
Mafuriko kutoka mbinguni: a.Mungu awalisha watu wake kwa mana na kwale kutoka mbinguni
|
Kutoka 15:22-27 Kutoka 16:1-21 Wazee na Manabii uk. 291- 295 |
WIKI YA 11 |
Mali ya Mungu: a. Zaka na sadaka b. Miili yetu c. Mazoezi |
|
WIKI YA 12-13 |
Anguko la Yeriko a. Wapelelezi watatu b. Wapelelezi wawili c. Rahabu awaokoa wapelelezi d. Anguko la Yeriko |
Joshua sura ya 5:10-15 Joshua sura ya 6 Wazee na Manabii uk. 487 – 493 Waebrania 11:30 |
WIKI YA 14 -16 |
Samson: Mtu ambaye hakuwahi kunyoa a. Kuzaliwa kwa Samsoni b. Mpango wa Mungu kwa Samsoni kuwaokoa watu wake c. Kifo cha Samsoni |
|
WIKI YA 17 - 18 |
Amri kuu za Mungu: a. Musa akutana na Munu katika mlima Sinai b. Mungu atoa mbao mbili za mawe zenye amri za Mungu c. Amri kumi za Mungu |
Kutoka 20:12-17 Wazee na Manabii uk. 308-309 |
WIKI YA 19 -20 |
Gidioni a. Mungu amwita kijana Gidioni b. Gidioni apigana vita akiwa na watu 300 |
Wafalme sura ya 7 Wazee na Manabii uk. 546-556 |
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-2 |
Kisa cha Ayubu a. Ayubu na utajiri wake b. Ayubu apoteza mali zake zote c. Ayubu augua d. Ayubu abarikiwa tena e. Uwakili: Vyote viijazavyo ni mali ya Bwana |
Ayubu sura ya 1-4 |
WIKI YA 3-4 |
Nabii aliyekimbia a. Yona aitwa na Mungu b. Yona aitwa ajaribu kumkimbia Mungu c. Yona katika tumbo la samaki d. Samaki amtapika Yona e.Hatuwezi kumkimbia Mungu |
|
WIKI YA 5-6 |
Kisa cha Eliya na mfalme Ahabu a.Nabii Eliya atumwa na Mungu kwenda kwa Ahabu b.Nabii Eliya na manabii wa Baali katika mlma Karmeli |
1 Wafalme sura ya 16 hadi 21 |
WIKI YA 7- 11 |
Vijana wanne wa kiyahudi huko Babeli: a. Jaribu la chakula kwa siku 10 b. Tanuru la moto c. Ndoto za Nebukadreza d. Mfalme aliyekula nyasi kwa siku e. Sherehe amayo haikukamilika f. Maadnishi ukutani g. Kutupwa katika tundu la simba |
Danieli sura ya 1 hadi 6 |
WIKI YA 12-13 |
a. Mwana mpotevu b. Kondoo mpotevu c. Lulu ya thamani |
Luka sura ya 15 |
WIKI YA 14 |
Kanuni ya muhimu: a. Kisa cha msamaria |
Luka sura ya 10:25-37 |
WIKI YA 15-16 |
Kisa cha Lazaro: a. Kifo ni nini? b. Yesu ana uwezo wa kufufua wafu c. Lazaro afufuliwa
|
Yohana sura ya 11 |
WIKI YA 17-18 |
Kutoka mteasji hadi mhubiri mashuhuri: a.Sauli katika barabara ya Dameski b.Sauli akutana na Mungu njiani c. Sauli awa Paulo mhubiri |
Matendo sura ya 9 |
WIKI YA 19-20 |
Esta awaokoa watu wake a. Esta awa malkia b. Esta aokoa maisha ya Mordekai c. Haman anyongwa |
Esta sura ya 1 hadi ya 8 |
SHULE YA MSINGI
DARASA LA KWANZA
MUHULA WA KWANZA
WIKI YA 1-4 |
Hapo mwanzo: a. Mungu na malaika b. Mungu ni nani? c. Utatu wa mbinguni i. Mungu Baba ii. Mungu mwana iii.Mungu Roho Mtakatifu
|
Mwanzo sura ya 1
Mathayo sura ya 6 |
WIKI YA 5-8 |
Kisa cha uumbaji a. Uwezo wa Mungu wa kuumba b. Juma la uumbaji c. Mungu apumzika siku ya saba d. Eden:Nyumbani kwa Adamu na Hawa |
Mwanzo sura ya 1 |
WIKI YA 9-13 |
Vita mbinguni a. Nafasi ya Lusifa b. Mwanzo wa ubinafsi c. Lusifa ashindwa na kutupwa duniani |
Wazee na Manabii uk.34-38 Tumaini kuu uk.392-498 Story of Redemption uk.13-15 Isaya 14:13 Ufunuo 12:7-9 Kumbukumbu 32:4 |
WIKI YA 14-16 |
Mibaraka ya Mungu: a. Maji b. Uzima c. Hewa |
|
WIKI YA 17-19 |
Anguko la mwanadamu a. Maelekezo ya Mungu kwa Adamu na Hawa b. Muongo mkuu c. Matokeo ya kuotii maelekezo ya Mungu d. Adamu na Hawa wafukuzwa Edeni e. Kifo na laana |
Mwanzo sura ya 2 Wazee na Manabii uk.36-38 Ezekieli 18:4 Mwanzo sura ya 3 1 Timotheo 6:15 1 Wakorintho 15:20-22 |
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Kaini na Habili: a. Tabia na kazi zao b. Mtu wa kwanza kufa na muuaji wa kwanza c. Mungu husikia na hujibu maombi yetu |
Mwanzo sura ya 4 Mwanzo 2:17 |
WIKI YA 5-6 |
Uwakili wa miili yetu a. Kuishi maisha yenye afya b. Pumziko na mazoezi |
|
WIKI YA 7-8 |
Kutembea na Mungu a. Henoko:Mtu aliyekwenda pamoja na Mungu b.Uaminifu wa Henoko |
Mwanzo sura ya 5 Wazee na Manabii sura ya 5 Story of redemption sura ya 6 |
WIKI YA 9-12 |
Kisa cha gharika a. Nuhu mtu pekee mwaminifu b. Mungu amwambia Nuu kutengeneza safina c. Nuhu atengeneza safina na kuhubir I kwa kwa miaka 120 d. Nuhu aingia kwenye safina pamoja na familia yake na wanyama safi e. Mvua kubwa yanyeha kwa siku 40 f. Nuhu atoka kwenye safina g. Upinde wa mvua h. Matokeo ya gharika i. baada ya gharika |
Mwanzo sura ya 6 Wazee na Manabii uk.90-95 Story of Redemption uk.62-64 |
WIKI A 15-19 |
Kisa cha jengo la ghorofa a. Mnara wa Babeli b. Mungu awatawanya wajenzi |
Mwanzo sura ya 11 |
DARASA LA PILI
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Familia ya Abraham Kuitwa kwa Abramu: a. Mungu amuita Abramu na kumulekeza kwenda katika nchi isiyojulikana b. Safari ya Abramu kwenda Kanaan kupitia Harani c. Abramu aenda Misri na kisha kurudi tena Kanaani
|
Mwanzo sura ya 12-14 |
WIKI YA 5-9 |
Upendo kwa wengine a. *Abrahamu amuokoa Luthu b. Luthu ahamia Sodoma c. *Abrahamu apata wageni d. Ombi maalumu la Abrahamu kwa ajili Luthu na Sodoma d. Kungamizwa kwa Sodoma e. Mke wa Luthu *Ni Abrahamu au Abramu?
|
Mwanzo sura ya 13, 18 na 19 Wazee na Manabii uk 138 -140 na uk. 156 - 169 |
WIKI YA 10-14 |
Ahadi za Mungu ni za kweli wakati wote: a. Mungu atoa ahadi ya motto kwa Abramu b. Hajiri na Ishmaeli c. Isaka, mtoto wa pekee d.Isaka amuoa Rebeka e.Jina la Abramu labadilika na kuwa Abrahamu |
Mwanzo sura ya 21, 23 na 24 Wazee na Manabii uk. 145- 147 na uk. 171-176
|
WIKI YA 15-19 |
Isaka na familia yake a. Ndugu wawili pacha waliokuwa tofauti b. Esau auza uzaliwa wa kwanza c. Yakobo amdanganya baba yake d. Yakobo akimbilia Harani: ngazi ndefu e. Maisha ya Yakobo huko Harani f. Yakobo aoa g. Yakobo arudi nyumbani:Ashindana na malaika:Jina la Yakobo labadilika kuwa Israeli
|
Mwanzo sura ya 23, 24, 26 na 27
Isaya 65:25 |
DARASA LA PILI
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Yakobo na familia yake huko Kanaani a. Watoto 12 wa Yakobo b. Yusufu: Mtoto anayependwa, muotaji c.Yusufu:Kutoka mtoto anayependwa hadi mtumwa |
Mwanzo sura ya 29, 37, 39, 41 na 45 Wazee na Manabii uk. 209 - 231 |
WIKI YA 5-8 |
Yusufu akiwa Misri: a. Yusufu katika nyumba ya Potifa b. Yusufu atafsiri ndoto ya Farao c. Yusufu awa kiongozi
Tufundishe namna ya kusali: Sala ya Bwana |
Mwanzo sura ya 37, 39, 41 na 45 Wazee na Manabii uk. 221-223
Mathayo sura ya 6 |
WIKI YA 9-12 |
Neno la Mungu a. Biblia b. Kuandikwa kwa Biblia c. Msingi wa ibada ya kweli d. Je, Mu ngu husikia na kujibu maombi? |
SDA Believe sura ya 1 |
WIKI YA 13-15 |
Yakobo na familia yake waenda Misri: a.Yakobo na familia yake wakaa Misri b.Mateso baada ya kuifo cha Yusufu |
Mwanzo sura ya 42 Kuotka sura ya 1 |
WIKI YA 16-20 |
Nguvu ya Mungu ya iokoayo na ilindayo: a. Kuzaliwa kwa Musa b.Maisha ya Musa katika nyumba ya Farao c. Musa aenda Midiani d. Maisha ya Musa utotoni akiwa na mama yake e. Musa aitwa na Mungu:Kichaka kinachowaka moto
|
Kutoka sura ya 2 na 3 Wazee na Manabii uk. 251- 256 |
DARASA LA TATU
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-5 |
Mungu aokoa watu wake: a. Musa na Haruni wakutana na Farao b. Mapigo kumi c. Kutoka Misri d. Kuishi maisha yenye afya:Mazoezi, Maji, Hewa safi, pumziko |
Kutoka sura ya 4 - 6 Wazee na Manabii uk. 257-265 Wazee na Manabii uk.265 -282 |
WIKI YA 6-9 |
Wokovu wa mwanadamu: a. Kuzaliwa kwa Yesu b. Kifo na kufufuka kwa Yesu |
Mathayo sura ya 1-2 |
WIKI YA 10-13 |
Safari ya waisraeli jangwani: a. Kuvuka bahari ya Shamu b.Wingu na moto c. Chakula kutoka mbinguni na maji kutoka kwenye mwamba |
Kutoka sura ya 14 – 16 Wazee na Manabii uk. 283-298 |
WIKI YA 14-17 |
Safari ya kutoka bahari ya Shamu hadi mlima Sinai: a. Amri kumi za Mungu b. Ndama wa dhahabu |
Kutoka sura ya 20 |
WIKI YA 18-20 |
Kunaguka kwa mji wa Yeriko: a. Wapepelelezi 12: Yoshua na Kalebu b. Musa aupiga mwamba mara mbili c. Kifo cha Musa |
Kutoka sura ya 20! |
DARASA LA TATU
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Sheria ya Mungu a.Musa aongea na Mungu katika mlima Sinai b.Amri kumi za Mungu c.Ibada ya sanamu/wanyama katika jamii za kiafrika e.Tufundishe namna ya kusali:sala ya Bwana |
Kutoka sura ya 20, 24 na 52 Wazee na Manabii uk. 308-330
Mathayo sura ya 6 |
WIKI YA 5-6 |
Matokeo ya kutokumtii Mungu: a. Taifa la Israeli walimuasi Mungu b. Mungu atuma nyoka wenye sumu c. Musa atengeneza nyoka wa shaba |
Hesabu sura ya 10, 11, na 21, 12 Wazee na Manabii uk.376 - 405 |
WIKI YA 7-8 |
Maisha ya Kikristo: a. Miili yetu kama hekalu la Roho Mtakatifu b. Chakua cha awali |
SDA Believe sura ya 21 1Wakorintho 6:15 |
WIKI YA 9-11 |
Yoshua ateuliwa: a. Makosa ya Musa na adhabu yake b. Joshua ateuliwa kuchukua nafasi ya Musa c. Kifo cha Musa |
Yoshua sura ya 1 Hesabu 20: 1-13 Wazee na Manabii uk.406-421 na 462-480 |
WIKI YA 12-13 |
Taifa la Israeli chini ya uongozi wa Yoshua: a. Kushambuliwa kwa mji wa Yeriko b. Kuvuka mto Yordani |
Wazee na Manabii uk. 481 – 486 Yoshua sura ya 1, 3-6 Wazee na Manabii uk. 487- 493 |
WIKI YA 14-16 |
Taifa la Israeli lapata mfalme: a.Wana wa Israeli wakataa utawala wa Mungu b.Wana wa Israeli wataka wawe na Mfalme: c. Familia zetu leo d.Mahusiano ya familia na jamii e. Familia ya kikristo/Familia ya Mungu |
1 Samweli sura ya 8 na 9 Wazee na Manabii uk. 592 -615 Elimu uk.45-50 |
WIKI YA 17-20 |
Familia na maisha ya familia: a. Familia katika muktadha wa kiafrika b. Familia ya awali c. Familia zetu leo d. Mahusiano kati ya familia na jamii e. Familia ya kikristo/Familia ya Mungu |
SDA believe sura ya 2 Mwanzo 12:3 Waefeso 3:15 |
DARASA LA NNE
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Kisa cha Daudi: a. Daudi atiwa mafuta kuwa mfalme wa pili wa Israeli b. Daudi na Goliathi c. Daudi na Yonathani:Marafiki wa kweli |
1 Samweli 16 na 17 Wazee na Manabii uk.637-648, 660 – 664, 701-702 2 Samweli 5
|
WIKI YA 5-9 |
Maisha na kifo cha Yesu: a. Maisha ya awali ya Yesu b.Yesu aenda kanisani c. Ubatizo:Yesu abatizwa na Yohana d. Maana ya ubatizo na maandalizi kwa ajili ya ubatizo e. Ubatizo wa kuzamishwa majini f. Umuhimu wa ubatizo |
Mathayo? SDA believe sura ya 14 Mathayo sura ya 20 Matendo sura ya 13 Warumi 6:14 Waebrania 6:2 Waefeso 4:5 Wakolosai 2:12 SDA believe sura ya 4 |
WIKI YA 10-14 |
Kifo: a. Maelezo ya kiafrika kuhusu hali ya wafu b. Maelezo ya biblia kuhusu hali ya wafu c. Uwezo wa Yesu dhidi ya kifo |
SDA believe Zaburi 6:5 Yohana 11:11-14 1 Thesalonike 4:16-18
|
WIKI YA 15-19 |
a. Yesrusalemu: Mji mkuu wa Daudi b. Vita dhidi ya wafilisti c. Daudi apanga kujenga hekalu d. Dhambi ya Daudi e. Daudi na Nathan f. Dhambi kubwa ya Daudi |
2 Samweli 10 -12 Wazee na Manabii 714-726, 745-748 2 Samweli 19-24
|
DARASA LA NNE
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-5 |
a. Abrahamu: Rafiki wa Mungu b. Wageni wa Abrahamu c. Wageni wa Luthu d. Maisha ya Luthu akiwa Sodoma e. Sodoma yaangamizwa |
Mwanzo 15- 19 Wazee na Manabii uk. 136-140 |
WIKI YA 6-9 |
a. Isaka:mwana wa ahadi b. Mungu amjaribu Abrahamu c. Abrahamu ashinda jaribu |
Mwanzo 21 na 22 Wazee na Manabii uk. 145-147 |
WIKI YA 10-12 |
a. Mapacha waliokuwa hawafanani b. Kudanganya ili kupata mibaraka ya Mungu c. Mungu amsamehe Yakobo d.Yakobo asafiri kurudi nyumbani |
Mwanzo 25, 28-29 Wazee na Manabii uk. 179-181
|
WIKI YA 13-16 |
a. Yusufu:Muotaji b. Kutoka mtoto anayependelewa hadi mtumwa anayedharauliwa c. Kijana mdogo ambaye hangeweza kutenda dhambi c. Mwana mpotevu |
Mwanzo sura ya 37-39 Wazee na Manabii uk. 211-212 |
WIKI YA 17-19 |
a. Kutoka mtumwa hadi mtawala b. Ndugu wenye njaa c. Dhifa ya kushtukiza d. Yusufu ajitambulisha
|
Mwanzo sura ya 37 -39 Wazee na Manabii uk. 221 - 223 |
DARASA LA TANO
MUHULA WA KWANZA
WIKI YA 1-3 |
a. Siku za giza katika Israeli b. Eliya:Yahwe ni Mungu wangu c. Mungu amficha Eliya |
1 Wafalme 16, 17 na 18
|
WIKI YA 4 |
Mtumishi mchoyo |
2 Wafalme 5 |
WIKI YA 5-6 |
a.Yosia:Mfalme wa Yuda mtoto b.Yosia aliongoza taifa kwa Mungu |
2 Wafalme 22 2 Wafalme 23 |
WIKI YA 7-9 |
a. Ndoto iliyosahaulika b. Tanuru la moto |
Danieli sura ya 2 na ya 3 |
WIKI YA 10-13 |
a. Mvulana kutoka Nazarethi b. Malaika waimba c. Mamajusi wa Mashariki d. Kukimbilia Misri e. Yesu katika pasaka yake ya kwanza |
Luka sura ya 1 na ya 2 |
WIKI YA 14-17 |
a. Yesu aenda kisimani b. Yesu apumzika katika kisima cha Yakobo c.Yesu aponya akiwa mbali d. Sabato yenye shuhuli nyingi e. Kipofu mwombaji apata hitaji lake f. Dhoruba katika ziwa Galilaya g.Yesu atumia chakula cha mchana cha mvulana h. Mmoja ashukuru badala ya kumi |
Yohana sura ya 1, 4 na 6 Marko sura ya 1, 4 na 4 Luka sura ya 7
|
WIKI YA 18-19 |
a. Huduma ya Yesu katika hekalu la mbinguni b. Kuja kwa Yesu mara ya pili c. Kifo na ufufuo |
Adventist believe |
DARASA LA TANO
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-5 |
Uaminifu na mkono wa Mungu wa ulinzi:Danieli, Meshaki, Shadraka, Abednego wakiwa Babeli a. Jaribu juu ya chakula b.Shadraka, Meshaka na Abednego katika tanuru la moto: Jaribu juu ya ibada ya kweli c.Danieli katika tundu la sindano: Maombi na ushuhudiaji d. Umuhimu wa maombi na matokeo yake |
SDA believe sura ya 21 Mwanzo sura ya 1 Njia Salama uk…. |
WIKI YA 6-9 |
Maisha ya baadaye ya Abrahamu na Lutu a. Njaa katika nchi ya Kaanani:Abrahamu ahamia Misri b. Abrahamu atengana na Lutu c. Lutu ashambuliwa na kuokolewa na Abrahamu |
Mwanzo sura ya 14 |
WIKI YA 10-14 |
Lutu akiwa Sodoma: a. Abrahamu atembelewa na wageni watatu b. Ombi la Abrahamu kwa ajili ya Lutu c. Kuangamizwa kwa Sodoma d. Lutu na familia yake waokolewa e. Mke wa Lutu ageuka kuwa nguzo ya chumvi
|
Mwanzo sura ya 18 na 19 Wazee na Manabii uk.138-140 na 156-167 |
WIKI YA 15-20 |
Ubatizo a. Yesu abatizwa na Yohana mbatizaji b. Maana ya ubatizo c. Maandalizi ya ubatizo wa kweli d. Ubatizo wa maji mengi
|
Mathayo sura ya 20 Warumi 6:4 Matendo sura ya 13 Waebrania 6:2 Waefeso 4:5 Wakolosai 2:12 SDA believe sura ya 14
|
DARASA LA SITA
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-4 |
Kuzaliwa kwa Isaka na utii wa Abrahamu: a. Kuzaliwa kwa Isaka b. Mungu amjaribu Abrahamu kwa mtoto wake wa pekee |
Mwanzo 21:35 Wazee na Manabii uk.145-147 |
WIKI YA 5-9 |
Ndoa na familia ya Isaka: a. Isaka amuoa Rebeka b. Maisha yaawali ya ndugu pacha:Esau na Yakobo c. Yakobo amdanganya baba yake na aondoka nyumbani c. Njia ndefu kuelekea kwenye usalama d. Yakobo akiwa Harani e. Safari ya Yakobo kurudi nyumbani |
Mwanzo sura ya23 na 24 Wazee na Manabii uk. 171-176 Isaya 65:24 |
WIKI YA 10-13 |
Sabato: a. Asili ya Sabato b. Sabato kama kumbukumbu ya uuumbaji c. Siku ipi ya wiki ndiyo Sabato? d. Namna ya kutunza Sabato e. Asili ya utunzaji wa Sabato f. The ten commandments |
Mwanzo sura ya 2 Luka 4:16 Yohana 7:10-12 Isaya 56:1-8 Kutoka 16:22-30 Isaya sura ya 58 Mathayo 28:1 Matendo 20:6-16 SDA believe sura ya 19 |
WIKI YA 14-16 |
Taifa la Isareli lakataa uongozi wa Mungu a. Taifa la Israeli baada ya kifo cha Yoshua b. Ombi la kuwa na mfalme c. Sauli awa Mfalme wa kwanza d. Taifa la Israeli chini ya mfalme Sauli e. Mwisho wa ufalme wa Sauli na kifo chake |
1 Samweli sura ya 8-11 |
WIKI YA 17-20 |
Mchungaji wa kondoo mdogo aliyekuja kuwa mfalme a. Maisha ya awali ya Daudi b. Daudi atiwa mafuta na nabii Samweli c. Daudi apigana na Goliathi d. Daudi na Yoanthani:marafiki wa kweli |
1 Samweli sura ya 16 2 Wafalme sura ya 2 |
DARASA LA SITA
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-3 |
Ndoa na familia: a. Ndoa ya awali iliyofanyika Edeni b. Mpngo wa Mungu kuhusu ndoa c. Ndoa katika mila za kiafrika d. Sala ya familia |
SDA Belive sura ya 22
Njia salama |
WIKI YA 4-7 |
Mtu aliyeishi ndani ya samaki kwa muda wa siku 3: a.Yona aitwa na Mungu b. Yona ajaribu kumkimbia Mungu c. Safari ya Yona d. Yona atapikwa na samaki na aenda Ninawi |
Yona sura ya 1-4 |
WIKI YA 8-11 |
Uaminifu na imani:Kisa cha Ayubu a. Maisha ya awali ya Ayubu b. Ayubu ashtakiwa na shetani c. Jaribu la kwanza la Ayubu d. Jaribu la pili la Ayubu e. Ayubu abaki mwaminifu kwa Mungu wake f. Ayubu afnikiwa tena |
Ayubu sura ya 1-2 |
WIKI YA 12-14 |
MARUDIO |
|
WIKI YA 15-20 |
Esta amuokoa mjomba wake pamoja na wayahudi a. Esta awa malkia b. Esta aokoa maisha ya watu wake c. Mordekai apewa heshima d. kifo cha Hamani e. Mkono wa Mungu uokoao kwa wanaomtumaini na kumtegemea |
Esta sura ya 1-7 |
DARASA LA SABA
MUHULA WA KWANZA
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-3 |
Sisi ni mawakili wa Mungu: a. Uwezo ( Ability) b. Muda c. Mali |
SDA Believe sura ya 20 |
WIKI YA 4-6 |
a. Mfano wa talanta b. Kafara na sadaka katika ibada za asili za kiafrika c. Suala la utunzaji wa muda katika muktadha wa kiafrika |
|
WIKI YA 7-8 |
Maisha ya awali ya Yesu: a. Kuzaliwa kwa Yesu b. Masiha ya awali ya Yesu c. Yesu abatizwa d. Ubatizo wa kweli na maana yake e. Yesu ajaribiwa |
Mathayo sura ya 2 Tumaini la vizazi vyote |
WIKI YA 9-12 |
Huduma ya Kristo: a. Yesu aanza kuhubiri b. Kuitwa kwa wanafunzi wa kwanza c. Yesu afundisha kwa mifano d. Hubiri la mlima i e. Yesu aponya wagojwa na kufanya miujiza f. Yesu azungumzia ufalme wa mbinguni i. Vazi la harusi ii. Wanawali kumi iii. Sifa za heri |
Mathayo sura ya 4 na 5 |
WIKI YA 13-14 |
Kifo cha Yesu: a. Yesu asalitiwa b. Ashtakiwa na kuhukumiwa c. Yesu asulubiwa d. Kufufuka kwa Yesu e. Umuhimu wa kifo na ufufuko wa Yesu f. Imani za kiafika kuhusiana na hali ya wafu |
|
WIKI YA 15-17 |
Wokovu: a.Kisa cha Zakayo b.Kijana tajiri c.Kisa cha Lazaro d.Yohana mbatizaji |
Luka sura ya 18 na 19 Yohana sura ya 3
|
WIKI YA 18-20 |
Vijana watumwa wasimamia imani yao a. Kisa cha Yusufu akiwa Misri b. Kutoka gerezani hadi katika ikulu ya mfalme c. Danieli, Meshaki, Shadraka na Abedinego wakiwa Babeli d. Unaweza kusimama leo |
|
DARASA LA SABA
MUHULA WA PILI
WIKI |
MADA |
VITABU VYA REJEA |
WIKI YA 1-2 |
Mlima Sinai na agano: a. Amri kumi za Mungu b. Ndama wa dhahabu c. Kutengenzwa kwa patakatifu d. Kazi za patakatifu e. Samani (fenicha) za patakatifu |
Kutoka sura ya 20, 25-27
|
WIKI YA 3-5 |
a. Huduma ya Hekaluni b. Kuhani alimwakilisha Kristo c. Mungu aonyesha mpango wake wa ukombozi |
Kutoka sura ya 25-31 Wazee na Manabii uk. 347-349 Ufunuo 24:5-9 |
WIKI YA 6-8 |
Musa amaliza huduma yake: a. Musa afanya kosa b. Mrithi wa Musa c. Kifo cha Musa |
Kumb. Sura ya 31-34 Wazee na Manabii uk. 462-480 |
WIKI YA 9-13 |
Kuingia na kuishi Kanaani: a. Kutoka Kadeshi Barnea hadi Yordani b. Nchi ya Kanaani au Palestina c. Kuingia kwa wana wa Israeli katika nchi ya ahadi d. Kuanguka kwa mji wa Yeriko |
Wazee na Manabii uk. 482 Yoshua sura ya 5 na 6 |
WIKI YA 14-17 |
a.Yoshua katika kuingia Kanaani b.Kugawanywa kwa nchi c.Kifo cha Yoshua |
Yoshua sura ya 9, 14-21 Wazee na Manabii uk. 505-517 Hesabu sura ya 30-34 |
WIKI YA 18-20 |
Waamuzi: a.Waamuzi wa awali b.Debora na Baraka c. Gidioni d.Yefta e. Samsoni f. Samweli |
1 Waamuzi sura ya 5-6, 13-16 Wazee na Manabii uk.545-547, 560-582 Ruthu sura ya 1-4 1Samweli sura ya1-3 |