Majukumu ya Karani wa Kanisa
- Kuandaa mikutano ya baraza la kanisa na mkutano mkuu kwa kuwapa taarifa wajumbe juu ya kuwepo kwa mkutano husika mapema kama inavyoagizwa na mwongozo, na kuwaalika kuhudhuria katika mkutano huo akitaja mahali na wakati wa kuanza kwa mkutano wenyewe, na ikibidi ajenda za mkutano.
- Kuandika na kutunza kumbukumbu zote za vikao vya mabaraza ya kanisa na mkutano mkuu kwa kuzingatia utaratibu wa uandishi unaoelekezwa.
- Kuandika na kutunza kumbukumbu sahihi za washiriki wanaoingia na kutoka wakati wote na kutuma taarifa ya takwimu kunakohusika kila mwisho wa robo (Machi, Juni, Septemba, na Disemba)
- Kutunza orodha sahihi ya mahudhurio ya washiriki kwenye Meza ya Bwana ya kila robo.
- Kutayarisha na kukabidhi vyeti vya ushirika, vyeti vya ubatizo, na vyeti vya kubariki watoto, kwa wahusika kwa wakati.
- Kupokea maombi ya uhamisho kwa wanaotaka kuhama, na kuyawasilisha katika vikao husika kwa maamuzi, kabla ya kuyatuma kwa makanisa husika. Atatakiwa kuanisha kama jina limetumwa; (a) ndani ya mtaa (b) nje ya mtaa, ndani ya konferensi. (c) nje ya konferensi, ndani ya Union au (d) Nje ya Union.
- Kuandika barua ya utambulisho na kuikabidhi kwa wanaotaka kusafiri kwa muda usiozidi miezi mitatu.
- Kuandika fomu za miito kwa agizo la bodi ya wazee wa kanisa, au baraza la kanisa, au Mkutano mkuu kutegemeana na unyeti na uharaka wa jambo lenyewe. Wito utaainisha kuwa umetumwa; (a) ndani ya mtaa (b) nje ya mtaa, ndani ya konferensi. (c) nje ya konferensi, ndani ya Union au (d) Nje ya Union.
- Kuwasiliana na washiriki walio mbali waliokaa zaidi ya miezi mitatu akiwajulisha mipango ya maendeleo na wajibu wao wa kuendelea kulichangia kanisa kwa michango, sadaka, na zaka zao.
10. Kutayarisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka akianisha mahitaji ya vitendea kazi na gharama zingine muhimu za ofisi.
SIFA ZA KARANI WA KANISA
Mwenye kiwango cha elimu ya kutosha kuweza kuyamudu majukumu ya ukarani