UWEKWAJI WAKFU ALBUM NA UZINDUZI WA UWANJA
Tarehe 30/03/2019 ilishuhudia uwekwaji wakfu wa album ya kwanza ya Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tegeta. Tukio hili lilifanywa na Mwenyekiti wa Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT), Mchungaji Joseph Mngwabi, kwenye ibada ya siku ya Sabato.
Pamoja na kuweka wakfu album, Mwenyekiti Mngwabi ambaye pia ndiye Askofu Mkuu wa Jimbo, alizindua eneo la kanisa lilionunuliwa kutoka kwa jirani kwa gharama ya Ths. milioni 100 kupitia michango ya washiriki wenyewe. Katika tukio hilo ofisi ya Konferensi alichangia ununuzi wa seti moja ya wireless microphone itakayotumika kwenye kanisa la Watoto Tegeta.
Kanisa la Tegeta linakusudia kujenga Kanisa linalokidhi mahitaji ya idadi ya washiriki wanaozidi kuongezeka na miundo mbinu mingine kukidhi mahitaji ya jamii inayowazunguka.

Mwenyekiti Mngwabi akiiangalia albamu inayowekwa wakfu kabla ya kuanza mahubiri ya Sabato hiyo. Tukio hili na matukio mengine ya siku hiyo yalirushwa mbashara kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.
.jpeg?thumbnail=original&1555593208)
Mwenyekiti Mngwabi akikata akifungua albamu kuashiria kuanza kutumika kwa albamu hiyo na huku Mhazini wa Konferensi ndugu Enock Rabieth aliyeandamana na Mwenyekiti akishuhudia. Katika ziara hii Mwenyekiti aliandamana na Mhazini wa Konferensi ndugu, Enock Rabieth, Mkurugenzi wa Uwakili na ATAPE mchungaji Jonas Singo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Chaplensia, mchungaji William Izungo, na Dereva wa Mwenyekiti ndungu Safiel Mbwambo.

Wanakwaya wa Tegeta Adventist Church wakishuhudia tukio la kuwekwa wakfu kwa album yao ya kwanza kwa shauku.

Mtoto aliyesoma risala kwa niaba ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tegeta akipeana mikono na mwenyekiti wakati wa kukabidhi risala hiyo huku viongozi walioandamana na mwenyekiti wakishuhudia. Mtoto huyu alisoma risala hiyo kwa ufasaha na umakini mkubwa uliowashangaza wengi.

.jpeg?thumbnail=original&1555593286)
Mchungaji Joseph Mngwabi akisoma Maandiko wakati wa uzinduzi wa kiwanja cha nyongeza cha kanisa kilichopatikana kupitia michango ya washiriki wenyewe.

Mchungaji na Askofu Joseph Mngwabi akiomba kwa ajili ya kuzindua na kuweka wakfu kiwanja cha Kanisa la waadventista wa sabato Tegeta tarehe 30.03.2019